Disemba 19 hadi 25 mwaka huu, Mchungaji Josephine Miller (wa tatu kushoto) kutoka Marekani alikuwa akifundisha na kuhubiri katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Baada ya huduma hiyo, jana Disemba 27, wenyeji wake (pichani) wakiongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (wa sita kulia) na Mama Mchungaji Mercy Kulola (wa tano kulia), walimtembeza Mchungaji Miller katika hifadhi ya Taifa Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika fidhahi hiyo.
Imeandaliwa na George Binagi, Picha na Jorum Samwel
Wanaumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, baada ya kuwasili katika hifhadhi ya Serengeti
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifurahia uwepo wao ndani ya hifadhi