Waumini wawili wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabsaba Ilemela Jijini Mwanza, Bwana Robson Mkesha Baliyanga (katikati) na Miss Penina Mkama (kushoto) leo Septemba 04,2016, wamefunga ndoa (pingu za maisha) takatifu.
Ibada ya ndoa hiyo imefanyika katika Kanisa hilo na kuuongozwa na Mchungaji Kiongozi, Dkt.Daniel Moses Kulola. Tafrija inafanyika jioni kwenye ukumbi wa Maendeleo House uliopo Iloganzara Jijini Mwanza.
"Mungu akasema;
"Mungu akasema; Si vyema mtu huyu awe peke yake, Nitamfanyia mtu wa kufanana naye". Mwanzo 2:18
Bwana harusi akifanya utambuzi wa mkewe, kabla ya ndoa kufungwa
Maharusi wakiingia kanisani
Maharusi wamependeza vyema
Ujumbe umepokelewa duniani na mbinguni.