Mshindi wa shilingi Milioni 100 kutoka Jijini Mwanza katika promosheni ya M-Power inayosimamiwa na kampuni ya simu ya Vodacom, Mama Paulina Kulwa (kushoto), akiwa na mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola wakati wa kukabidhiwa hundi yake.
Mama Paulina Kulwa (58) ni...
Mama Paulina Kulwa (58) ni mtumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kitengo cha utawala, anasema alipigwa butwaa baada ya kupigiwa simu kutoka Vodacom makao makuu Jijini Dar es salaam kwamba amejishindia shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Vodacom M-Power ambapo awali alijua ni matapeli.

Baada ya kufika ofisi za Vodacom Jijini Mwanza na hatua zote kufuatwa na kuonekana ni kweli ameshinda fedha hizo, jumapili iliyopita alimshukuru Mungu mbele ya kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza analosali na kusema kwamba kufanya kazi kwa bidii pamoja na kumtumikia Mungu kwa uaminifu kumesababisha aibuke na ushindi huo.
"Nimefanya kazi miaka yote kwa uaminifu licha ya vishawishi vingi hadi nimekuwa nikitunukiwa ufanyakazi bora. Pia nimekuwa nikiwasaidia watu mbalimbali ikiwemo kusomesha watoto yatima na kumtumikia Mungu kwa uaminifu. Sasa Mungu amenikumbuka na mimi". Alisema huku akishangiliwa na waumini wa kanisa la EAGT Lumala Mpya.
Ajabu ni kwamba mjukuu wa mama huyu ndiye aliyechukua simu na kushiriki bahati na sibu ya Vodacom M-Power ambapo alitumia awali aliibua mzozo baada ya kukopa 16,000 kwenye M-Power na zote kuzitumia kwenye promosheni hiyo.
Mwandishi wa habari hii, George Binagi (kushoto), akisalimiana na Mshindi wa promosheni ya M-Power inayosimamiwa na kampuni ya simu ya Vodacom, Mama Paulina Kulwa (kulia).