Jumapili Oktoba 09, 2016 katika Kanisa la "EAGT Lumala Mpya International Church" Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, linatarajiwa kufanyika tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo...
Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, amewahisi watu wote
kufika kwenye tamasha hilo kwani kwenye kusifu na kuabudu, ana uhakika
wa kuisikia sauti ya Mungu na huwa huru na kujitenga na dhambi
ikizingatiwa kwamba kuna nguvu ya Mungu kwenye kusifu na kuabudu.
Mratibu wa tamasha hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana, Max Kemmy, amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake na kwamba litaanza kuanzia majira ya saa nane kamili mchana likiwa na ujumbe usemao, "Njoo Tuabudu Pamoja".