Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (kushoto) amekutana na mtoto mtanzania aliyeigiza sinema ya The Real MVP nchini Marekani.
Dkt.Kulola alikutana na mtoto huyo, Evan Byarushengo (7 kulia), alipokuwa Texas nchini Marekani kwa ajili ya huduma ya neno la Mungu ambapo Mchungaji Kulola amewasili leo Jijini Mwanza.
Mtoto huyo (kulia) amekuwa miongoni mwa watoto wachache duniani hususani kutoka mataifa ya Afrika, kuweza kushiriki katika sinema za Hollywood nchini Marekani akiwa na Mastaa mbalimbali.
Mchungaji Kulola akiwa pamoja na wafamilia ya mtoto huyo nchini Marekani.