Disemba 19 hadi 25 mwaka huu, Mchungaji Josephine Miller (wa tatu kushoto) kutoka Marekani alikuwa akifundisha na kuhubiri katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Baada ya huduma hiyo, jana Disemba 27, wenyeji wake (pichani) wakiongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (wa sita kulia) na Mama Mchungaji Mercy Kulola (wa tano kulia), walimtembeza Mchungaji Miller katika hifadhi ya Taifa Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika fidhahi hiyo.
Imeandaliwa na George Binagi, Picha na Jorum Samwel
Wanaumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, baada ya kuwasili katika hifhadhi ya Serengeti
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifurahia uwepo wao ndani ya hifadhi
Mwanahabari wa Lake Fm Mwanza akiwa na Waumini wa EAGT Lumala Mpya
Safari ya kuanza kutembelea hifadhi ya Serengeti
Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani (kulia) akifurahia uwepo wake ndani ya hifadhi ya Serengeti. Kushoto ni Mwanahabari na Blogger wa Lake Fm Mwanza, George Binagi
Wanyama mbalimbali wakiwemo pundamilia na nyati wakiwa kwa makundi ndani ya hifadhi ya Serengeti
Pundamilia, nyumbu na nyati wakiwa kwenye makundi ndani ya hifadhi ya Serengeti
Nyani ndani ya hifadhi ya Serengeti
Mama na Mwana
Twiga na upendo wao, hawaachani
Twiga na upendo wao, hawaachani
Matukio yakiendelea kunaswa katika eneo la Viboko na Mamba
Tembo ndani ya hifadhi ya Serengeti
Mfalme Simba akiwa anapumzika
Simba mjamzito
Hili ni daraja la waya ndani ya hifadhi ya Serengeti, ni katika eneo lenye Viboko wengi. Kulia ni Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola akiwa na Mwanahabari George Binagi
Mchungaji Josephine Miller akipanda daraja la kunesanesa, limetengenezwa kwa kama imara ya chuma
Mama Mchungaji, Mercy Kulola, akihofia daraja linavyonesa licha ya uimara wake
Chini ya daraja hili kuna wanyama wengi aina ya Viboko na hata Mamba
Daraja la kunesanesa
Ni muda wa chakula ndani ya hifadhi ya Serengeti huku pia Watalii wa Ndani na Watalii wa Nje, wakifurahia pamoja uzuri wa hifadhi ya Serengeti.
Watanzania wametakiwa kuongeza hamasa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ikiwemo hifadhi za Taifa ili kufurahia rasilimali walizotunukiwa na Mwenyezi Mungu.
Mchungaji Josephine Miller kutoka nchini Marekani aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vya wanyama katika hifadhi hiyo.
Alisema alipokuwa katika hifadhi mbalimbali barani Afrika ikiwemo za Afrika Kusini na Zimbabwe, alikuwa akisikia kuhusu uzuri wa hifadhi ya Serengeti hivyo amefurahia kutembelea hifadhi hiyo akisema kwamba hilo lilikuwa ni chaguo lake la pili baada ya kuonana na watu wa bara la Afrika.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Kulola, alisema ni vyema Mamlaka ya Hifadhi za Taifa TANAPA ikaongeza hamasa kwa Watanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuukuza zaidi utalii wa ndani huku akiomba suala la miundombinu ya barabara kuboreshwa ili watalii.
Kumbuka Mtanzania hulipa Tsh.11,800 pamoja na VAT kwa mtu mzima ili kuingia katika hifadhi ya Serengeti. Wageni hulipa dolla 70 ikikadiliwa kuwa Tsh, laki moja na elfu hamsini na nne. Hakika watanzania wanayo furusa kubwa kutembelea vivutio vya vya utalii.