Jana Julai 29,2017 Mchungaji Mercy Kulola akiwa kwenye mahafali yake baada ya kuhitimu masomo ya biblia ngazi ya Diploma, katika chuo cha Biblia St.Paul Jijini Mwanza.
Baada ya mahafali yaliyofanyika viunga vya chuo cha St.Paul, waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, walimuandalia hafla ya kumpongeza iliyofanyika kanisani hapo majira ya jioni. BMG tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Mchungaji Mercy Kulola kwa hatua hiyo muhimu katika maisha yake.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola akimpongeza mkewe, Mchungaji Mercy Kulola kwa kuhitimu elimu yake ya uchungaji ngazi ya Diploma, katika Chuo cha Biblia St.Paul Jijini Mwanza
Ndugu, jamaa na marafiki kwenye picha ya pamoja
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola na mkewe Mchungaji Mercy Kulola kwenye hafla ya jioni
Wasaa wa kukata keki ya pongezi
Muda wa kulishana keki ishara ya upendo
Mchungaji Mercy Kulola akimlisha keki mzee wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya
Mwenyekiti wa kamati ya sherehe akipokea keki
Joram Samweli kutoka EAGT Lumala Mpya akifungua shampeni
Mhitimu Mchungaji Meryc Kulola, akimnywesha shampeni mmewe Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola
pongezi
Pongezi
Muda wa zawadi
Zawadi
Salamu za pongezi kutoka kwa Katibu wa kwaya ya Havillah
Zawadi wa Mchungaji Mercy Kulola baada ya kuhitimu masomo yake ya uchungaji
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akitoa salamu zake na kumpongeza mkewe kwa kuitikia sauti ya Mungu na kwenda kusomea uchungaji bila kushinikizwa na mtu yeyote
Mchungaji Mercy Kulola akitoa shukurani zake kwa waumini wa kanisa la EAGT Lumala Mpya kwa kumuandalia halfa ya kumpongeza baada ya kuhitimu masomo yake ya uchungaji ngazi ya Diploma
Wazee wa Kanisa na kulia ni mwanafamilia
kumbukumbu adhimu
Baadhi ya waumini waliohudhuria hafla hiyo
Mchungaji Mercy Kulola (katikati) alihitimu masomo yake ya uchungaji na kutunukiwa ufaulu wa juu katika Chuo cha St.Paul Jijini Mwanza jana Julai 29,2017