Katika kuonesha kuwakumbuka watu hawa muhimu katika Tanzania, mtoto wa aliyekua Askofu Mku wa kanisa la EAGT nchini Tanzania Dr.Moses Kulola, afahamikaye kama Mchungaji Dr. Daniel Kulola amepost katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook picha akiwa na baba yake "Kulola " na aliyekua Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta siku walipokutana pamoja uwanja wa ndege katika safari .
Itakumbukwa kuwa Askofu Moses Kulola alifariki dunia mwaka 2013 akiacha alama kama Baba wa Injili nchini Tanzania na kiongozi aliyewalea kihuduma watumishi wengi wakubwa na maarufu , huku aliyekua Spika mstaafu Samuel Sitta amefariki mwezi November mwaka huu 2016 na kuacha simanzi nzito kwa taifa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa taifa la Tanzania katika utumishi wake katika serikali.