
Pastor na mwinjilisti wa Kimataifa ambaye ndiye mtoto pekee
ambaye amerithi huduma na majukumu ya askofu mkuu marehemu Dr Moses
Kulola aitwaye Dr. Daniel Moses Kulola amepata mwaliko wa kuelekea Washington
Dc Marekani.Ataanzia Boston,kisha Washington DC,Alabama,Dallas,Texas Austin,New york na mahali pengine hakuweza taja kwa huduma ya mwezi mmoja na nusu kuanzia 17 Desemba hadi 30
january 2014.
Akieleza juu ya safari hii kubwa kuwa muda mwingi amekuwa
akialikwa kwenda marekani lakini kuna mambo mengi yalikuwa yanaingilia kati
kuwa kizuizi. Lakini baada ya mazishi ya baba yake ambaye ni baba yetu sote
ameona ni vyema kusafiri kwenda katika huduma maana wengi wamekuwa wakimuhitaji
katika nchi hiyo iliyojaa mambo mengi.
Dr. Daniel kulola amekuwa ni moja wa wahubiri wachache ambao
wamepata neema ya kipekee ya kwenda kuhubiri katika nchi nyingi zilizoendelea
kama uingereza, ujerumani, Dernmark na kwingineko kwingi. Na taarifa ambazo
tumeendelea kuzifuatilia kwa karibu ni kuwa kwa sasa ndiye mhubiri pekee ambaye
ameweza kutunza na kuzifuata nyayo za askofu mkuu marehemu Moses kulola na pia
ndiye mwenye kibali kikubwa hasa katika makanisa ya EAGT.
Nikiongea naye anasema amealikwa na kanisa la Bethel kingdom
church la washington Dc linaloongozwa na askofu Merchizedek pia ataendelea
kuhudumu maeneo mbali mbali pamoja na kanisa la Miracle Life worldwide la jimbo
la Texas, pia atafika New York.
pamoja na yote kipindi atakwenda peke yake tofauti na
ilivyozoeleka kila anaposafiri huwa anasafiri na mkewe Mercy Daniel katika
huduma zake zote akifuata nyayo za baba yake.
alitoa pia dokezo atakapo rudi atafanya uzinduzi wa kitabu
cha maisha ya mzee Moses kulola ambacho kwa sasa kimekamilia kwa asilimia kama
97. Kimeandaliwa kama kwa miaka 2 hadi na nusu hivi na msimamizi wa kitabu
hicho ni yeye mwenyewe Dr. Daniel kulola.
alimalizia kwa kusema anahitaji maombi ya wana injili wote
wawe naye hasa katika kipindi hiki cha mpito pia alisema ataondoka Tanzania 15
Dec na kufika washington Dc 16 Dec na kuanza huduma ambayo itampeleka hadi 30
Jan 2014.
ukipenda maombi na ushauri pia simu yake iko hewani +255 767
749040 na +255 784 749040

Hapa Dr Kulola akiwa kwenye mikutano tofauti akinena
neno la uzima kwa nguvu


Anakabidhiwa kijiti cha injili kuhubiri bila woga injili ya Yesu kwa mataifa yote


