Wednesday, 22 February 2017

WENGI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Zoezi la upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani linalofanyika kwa siku tangu kuanzia jana, linaendelea katika viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela.

Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) amebainisha kwamba jana zaidi ya wananchi 150 walijitokeza kupima afya zao ambapo zaidi ya 70 walihudumiwa na kurejea nyumba.

Alisema zoezi hilo limejikita kwenye uchunguzi wa afya ya uzazi, kisukari, presha pamoja na uzito likiongozwa na wataalamu wa afya kutoka Canada wanaosaidizana na wataalamu wazawa na muda ni kuanzia saa mbili kamili asubuhi.

Umati wa akina mama waliojitokeza kwenye zoezi la upimaji afya bure katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya
Zoezi la kuchukua taarifa likiendelea kwa umakini
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana na linasimamiwa na wataalamu wa afya kutoka Canada
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Kwa wale watakaobainika kuwa katika hali ya uchunguzi zaidi watasaidiwa kufikishwa kwenye hospitali za rufaa ili kuhudumiwa.
#BMG
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates