Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Martha Baraka (katikati), kwaya na waimbaji mbalimbali wamepamba vyema Mkutano Mkubwa wa Injili unaofanyika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Ilemela Jijini Mwanza.
Waimbaji wengine kwenye mkutano huo ni pamoja na Stella Ngumba, Ajuaye Onesmo na kwamba kadhaa ikiwemo EAGT Kaangaye na wenyeji New Salvation na Havilah Gospel Singers.
Watumishi wa Mungu kutoka Canada ambao ni Fred Mitchell, Karlin Mitchell, Joyce Dickson, Shirleen Weeks, Fredrica Walters na Barry Walters kwa pamoja na wenyeji wao chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola, wanahudumu katika mkutano huo ikiwemo kufanya maombezi ya nguvu kwa watu wote.
Mkutano huo ulianza jana Februari 22 na utarajiwa kufikia tamati jumapili hii Februari 26,2016 katika viwanja vya kanisa hilo kuanzia saa tisa kamili mchana.
#BMG
Mwimbaji Martha Baraka anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo "Nimekuja na Maua", akitumbuiza ipasavyo kwenye mkutano huo
Martha Baraka (kulia) pamoja na mmewe Baraka Mwakisepe (kushoto) wakihudumu kwenye mkutano huo
Miongoni mwa kwaya mwenyeji ya Havilah Gospel Singers ya EAGT Lumala Mpya ikihudumu kwenye mkutano huo
Miongoni mwa kwaya mwenyeji ya New Salvation ya EAGT Lumala Mpya ikihudumu kwenye mkutano huo
Miongoni mwa kwaya zilizoalikwa ya EAGT Kaangaye ya Jijini Mwanza ikihudumu kwenye mkutano huo
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akihudume kwenye mkutano huo
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia), akimkaribisha Mchungaji Fred Mitchell (kushoto) kutoka Canada ili kuhudumu kwenye mkutano huo. Katikati ni mkarimani kutoka EAGT Lumala Mpya.
Mchungaji Fred Mitchell (kushoto) kutoka Canada
Mchungaji Barry Walters (kulia) na mkewe Fredrica Walters (kushoto) wote kutoka Canada wakifuatilia mkutano huo.
Mchungaji Fred Mitchell (kushoto) na mkewe Karlin Mitchell (kulia) wote kutoka Canada wakiwa kwenye mkutano huo
Watumishi wa Mungu kutoka Canada, Shirleen Weeks (kushoto) pamoja na Joyce Dickson (kulia), wakifuatilia mkutano huo.
Mama Mchungaji, Mercy Kulola, pamoja na waumini wengine wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, wakiimba na kusifu kwenye mkutano huo
Mkutano huo huanza saa tisa kamili mchana, Usikose.