Jana jumapili Februari 12,2017, mdau George Binagi ambaye ni Mwanahabari wa Lake Fm Mwanza na Mwanablogu wa Binagi Media Group (kulia), alimtambulisha mchumba wake, Pendo Kisaka, mbele ya waumini wenzake wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza na kutangaza kusudio la harusi inayotarajiwa kufanyika mwezi March mwaka huu.
Picha na Robert Kasamwa
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) pamoja na Mama Mchungaji Mercy Kulola (kushoto), wakiongoza sala ya kuwaombea maharusi watarajiwa.
Bibi harusi mtarajiwa, Pendo Kisaka
Kutoka kushoto ni Mama Mchungaji Mercy Kulola, bibi harusi mtarajiwa Pendo Kisaka, Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola na bwana harusi mtarajiwa George Binagi
Bwana harusi mtarajiwa, George Binagi (kushoto) pamoja na best man wake, Joel Maduka (kulia) wa Storm Fm ya Geita na mtandao
Shukurani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wakiongozwa na kamati ya harusi, wanaohakikisha mipango yote ya harusi inakwenda kama ilivyokusudiwa, Mungu awabariki mno.