Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, akiwaombea waumini wa kanisa hilo kwenye ibada ya jana jumapili Februari 20,2017.
Kumbuka kuna mwendelezo wa mahubiri na mafundisho kutoka kwa watumishi wa Mungu kutoka Canada katika kanisa hilo kuanzia alhamisi iliyopita Februari 16 ambapo tayari makundi ya akina wanandoa, mama, wajane na vijana wamenufaika na mafundisho hayo.
Mafundisho mengine yanaendelea wiki hii kwa makundi mbalimbali ikiwemo mabinti hadi kesho februari 21 na baada ya hapo itafuata huduma ya vipimo bure pamoja na mahubiri kwa watu wote nje ya viunga vya kanisa hilo.
Watumishi wa Mungu kutoka Canada ambao ni Fred Mitchell, Karlin Mitchell, Joyce Dickson, Shirleen Weeks, Fredrica Walters na Barry Walters kwa pamoja na wenyeji wao watahudumu katika mahubiri hayo hadi tarehe 26.02.2017.
#BMGHabari
Mchungaji Barry Walters akihudumu jana katika kanisa la EAGT Lumala Mpya
Mtumishi wa Mungu kutoka Canada, Karlin Mitchell, akitoa salamu zake ndani ya EAGT Lumala Mpya
Mtumishi wa Mungu kutoka Canada, Shirleen Weeks, akitoa salamu zake ndani ya EAGT Lumala Mpya
Mtumishi wa Mungu kutoka Canada, Joyce Dickson, akitoa salamu zake ndani ya EAGT Lumala Mpya
Mahubiri na mafundisho kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya, pia hukujia #Live kupitia ukurasa wa Facebook wa mchungaji Daniel Moses Kulola. Mawasiliano 0767 74 90 40.