Majira ya saa mbili usiku jana, ujumbe mkubwa wa watumishi wa Mungu kutoka nchini Canada waliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza, kwa ajili ya huduma katika kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.
Pichani ni waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiongozwa na mchungaji wao Dkt.Daniel Moses Kulola (katikati), waliojitokeza kwenye mapokezi hayo.
Ujumbe wa watumishi wa Mungu kutoka Canada uliongozwa na Mchungaji Fred Mitchel pamoja na Mchungaji Fredrica Walters ambapo huduma ya semina imeanza hii leo Februari 16,2017.
Kutakuwa na semina na mafundisho kwa makundi mbalimbali ikiwemo akinamama, vijana, wanandoa na wajane hadi Februari 22 na baada ya hapo kutakuwa na mahubiri kabambe hadi Februari 26,2017 katika viunga vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya.
#BMG