Mchungaji wa Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, akizungumza kwenye ibada ya jana jumapili kwenye kanisa hilo ikiwa ni siku ya mwisho ya huduma iliyokuwa ikitolewa na watumishi wa Mungu kutoka Canada kuanzia Februari 16,2017.
Kuanzia Februari 16 hadi Februari 21,2017 watumishi hao walikuwa wakitoa semina kwa makundi mbalimbali ikiwemo wajane, wanandoa na vijana ambapo kuanzia februari 22 hadi 24 asubuhi waliendesha zoezi la upimaji wa afya bure na februari 22 hadi 26 kuanzia saa tisa mchana kulikuwa na mahubiri kwa watu wote.
Watumishi wa Mungu kutoka Canada walikuwa ni Fred Mitchell, Karlin Mitchell, Joyce Dickson, Shirleen Weeks, Fredrica Walters na Barry Walters. Katika huduma hiyo pia waimbaji mbalimbali akiwemo Martha Baraka walialikwa kuhudumu.
oKatika ibada ya jana, watumishi wa kanisa la EAGT Lumala Mpya, waliwatunuku zawadi watumishi hao ikiwa ni ishara ya kusema ahsante kwa huduma yao njema.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakimsikiliza Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola