Sunday 26 February 2017

WAUMINI WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA WAWATUZA WATUMISHI WA MUNGU KUTOKA CANADA.

Mchungaji wa Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, akizungumza kwenye ibada ya jana jumapili kwenye kanisa hilo ikiwa ni siku ya mwisho ya huduma iliyokuwa ikitolewa na watumishi wa Mungu kutoka Canada kuanzia Februari 16,2017.

Kuanzia Februari 16 hadi Februari 21,2017 watumishi hao walikuwa wakitoa semina kwa makundi mbalimbali ikiwemo wajane, wanandoa na vijana ambapo kuanzia februari 22 hadi 24 asubuhi waliendesha zoezi la upimaji wa afya bure na februari 22 hadi 26 kuanzia saa tisa mchana kulikuwa na mahubiri kwa watu wote.

Watumishi wa Mungu kutoka Canada walikuwa ni Fred Mitchell, Karlin Mitchell, Joyce Dickson, Shirleen Weeks, Fredrica Walters na Barry Walters. Katika huduma hiyo pia waimbaji mbalimbali akiwemo Martha Baraka walialikwa kuhudumu.

oKatika ibada ya jana, watumishi wa kanisa la EAGT Lumala Mpya, waliwatunuku zawadi watumishi hao ikiwa ni ishara ya kusema ahsante kwa huduma yao njema.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakimsikiliza Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola

Jana pia kuliwa na ibada ya kubariki watoto na hapa ni Mchungaji Dkt.Daniel Kulola na Mama Mchungaji Mercy Kulola wakiongoza ibada hiyo
Mama Mchungaji Mercy Kulola kwenye ibada ya kubariki watoto
Watumishi wa Mungu kutoka Canada ambao ni  Fred Mitchell (kushoto) na mkewe Karlin Mitchell (katikati). Kulia ni mtumishi wa Mungu Shirleen Weeks.
Watumishi wa Mungu kutoka Canada ambapo kutoka kushoto ni Mchungaji Barry Walters na mkewe Fredrica Walters. Watumishi wanaofuata ni Shirleen Weeks na Joyce Dickson.
Watoto wa wanaosoma shule ya awali ya EAGT Lumala Mpya na waalimu wao, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mungu kutoka Canada baada ya kuwatuza zawadi mbalimbali
Waimbaji wa kwaya ya Havillah ya EAGT Lumala Mpya wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mungu kutoka Canada baada ya kuwatuza zawadi mbalimbali
Watoto wa wanaosoma shule ya awali ya EAGT Lumala Mpya wakiwapa zawadi za asili wageni kutoka Canada
Mmoja wa akina mama akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kuwatuza wageni kutoka Canada
Mmewe Martha Baraka (kushoto) akitoa salamu za shukurani kwa mapokezi mazuri EAGT Lumala Mpya. Kulia ni mwimbaji Martha Baraka.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates