Sunday 22 January 2017

KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LAFURAHISHWA NA HUDUMA YA KWAYA YA EAGT KAANGAYE.

Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT Kaangaye kutoka Nyakato Jijini Mwanza, leo wamefanyika Baraka kubwa baada ya kuhudumu vyema katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

Waumini wengi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wamefurahishwa na huduma ya kwaya hiyo. Pongezi kubwa ziwaendee Mwenyekiti wa kwanya hiyo, Abednego Magesa na Mchungaji Samson Mniko kwa malezi mema yaliyofanikisha wanakwaya hao kumtumikia Mungu kwa bidii kubwa.

Sunday 15 January 2017

KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA, "KWELI MUNGU YUPO".


Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, kwenye ibada za leo jumapili, Januari 15,2017.

Kulikuwa na somo zuri liitwalo "KWELI MUNGU YUPO" kutoka kitabu cha 1-Wafalme 18 hivyo soma kwa kitabu hicho ili ujifunze zaidi kuhusiana na uwepo wa Mungu ukimtafuta kwa uaminifu.

Thursday 12 January 2017

MLIPUKO WA INJILI KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Ni Mlipuko wa Injili na Habari njema takatifu kwa watu wote.
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba, Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji na Mwinjilisti wa Kitaifa na Kimataifa, Dkt.Daniel Moses Kulola, linawakaribisha watu wote kwenye ibada zake.

Kila Jumapili ibada ya kwanza inaanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 1:00 kamili na ibada ya tatu ni saa 4:30 asubuhi huku ibada za katikati ya wiki zikifanyika jumatano na ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.

Sunday 8 January 2017

HII SI YA KUKOSA KUTOKA KWA MCHUNGAJI KULOLA WA EAGT LUMALA JIJINI MWANZA.

Usikose kufuatilia maombezi na ibada ya neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, mubashara (live) kupitia ukurasa wake wa facebook.

Ni kila siku ya alhamisi kuanzia saa nane kamili mchana kupitia ukurasa wake wa facebook wa Daniel Moses Kulola ambapo mahubiri na maombezi yatarushwa moja kwa moja (mubashara) kwa njia ya video.

Sunday 1 January 2017

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2017 KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Mchungaji wa Kanisa la "EAGT Lumala Mpya International Church"  lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola na Mama Mchungaji, Mercy Daniel Kulola, kwa niaba ya waumini wote, wanakutakia Sikukuu njema ya mwaka mpya wa 2017, uwe mwaka wenye Baraka tele kwako, Amen!
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates