Thursday 16 February 2017

UJUMBE MKUBWA WA WATUMISHI WA MUNGU KUTOKA CANADA WAPOKELEWA JIJINI MWANZA TAYARI KWA HUDUMA.

Majira ya saa mbili usiku jana, ujumbe mkubwa wa watumishi wa Mungu kutoka nchini Canada waliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza, kwa ajili ya huduma katika kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

Pichani ni waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiongozwa na mchungaji wao Dkt.Daniel Moses Kulola (katikati), waliojitokeza kwenye mapokezi hayo.

Ujumbe wa watumishi wa Mungu kutoka Canada uliongozwa na Mchungaji Fred Mitchel pamoja na Mchungaji Fredrica Walters ambapo huduma ya semina imeanza hii leo Februari 16,2017. 

Kutakuwa na semina na mafundisho kwa makundi mbalimbali ikiwemo akinamama, vijana, wanandoa na wajane hadi Februari 22 na baada ya hapo kutakuwa na mahubiri kabambe hadi Februari 26,2017 katika viunga vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya.
#BMG

 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates