Monday 25 December 2017

Kanisa la EAGT Lumala Mpya Mwanza Lafurahia Sikukuu ya Krismasi 2017

Ibada Maalumu ya Krismasi yanoga Kanisa la EAGT Lumala Mpya

Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji Kiongozi Dkt.Daniel Moses Kulola wameungana pamoja kusherekea ibada ya Krismasi kanisani hapo hii leo jumatatu Disemba 25,2017.
Ibada imekuwa ya kuvutia na baadaye imefuatiwa na chakula cha mchana. Fuatilia ilivyokuwa.
Bonyeza HAPA kwa habari zaidi

Sunday 24 December 2017

Salamu za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2018 kutoka Kanisa la Lumala Mpya

Ni jumatatu Disemba 25,2017 ambapo Wakristo kote duniani wanaungana pamoja kusherekea Sikukuu ya Krismasi ambayo ni kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Karibu kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza kupata salamu za Krismasi na mwaka mpya 2018.

Salamu za Krismasi na Mwaka Mpya kutoka kwa Mchungaji Daniel Kulola

Salamu za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2018 kutoka kwa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

Salamu za Krismasi na Mwaka Mpya kutoka kwa Mchungaji Mercy Kulola

Salamu za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2018 kutoka kwa Mchungaji Mercy Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

Tuesday 12 December 2017

Anayedai Kusababisha Ajali ya Daladala Ziwa Victoria Aokoka



Ikiwa ni miezi miwili sasa imepita tangu ajali hiyo mbaya itokee, mtu mmoja ameibuka na kukiri yeye na wenzake kusababisha ajali hiyo ambapo lengo ilikuwa kumchukua mshirika mwenzao aliyewasaliti aliyekuwa kwenye gari hiyo.

Sunday 12 November 2017

Ndoa ya Victor Misana wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya yafana

Ndoa ya Mr.Victor Misana pamoja na Miss Queen Mrema imefana leo Jumapili Novemba 12,2017 katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Wawili hao wote ni waumini wa kanisa hilo chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola. Baada ya ndoa hiyo, hafla inafanyika ukumbi wa New Mwanza Hote Jijini Mwanza usiku.
Bwana harusi Victor Misana, akimlaki bibi harusi Queen Mrema. Bwana harusi akithibitisha kuwa ndiye. Maharusi wakiingia kanisani, EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza. Maharusi wakiwa kanisani. Bwana harusi akimvisha pete mkewe.
Bibi harusi akimvisha pete mmewe. Maharusi wakionyesha pete za harusi. Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiwaombea maharusi. Mama Mchungaji Mercy Kulola pia akiwaombea maharusi. Kulia ni mwakilishi wa familia ya bibi harusi akimkabidhi kwa wakwe. Kulia ni mwakilishi wa familia ya bwana harusi akizungumza baada ya kumpokea bibi harusi.
Mr. & Mrs Victor Misana Maharusi pamoja na marafiki zao. Maharusi pamoja na wasimamizi wao. Mama Mchungaji Mercy Kulola (kulia) pamoja na wazazi wa bibi harusi.    

Wednesday 4 October 2017

WATUMISHI WA MUNGU WAPATA AJALI HIFADHI YA SERENGETI


Ni baada ya jumapili Oktoba Mosi watumishi hao wakiwemo kutoka Marekani kumaliza mkutano mkubwa wa injili jijini Mwanza.


Monday 2 October 2017

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO WATUMISHI WA MUNGU KUTOKA MAREKANI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani ikiongozwa na Mwinjilisti Rojas Matias, walipomtembelea ofisini kwake jana. 

Watumishi hao walikuwa na mkutano mkubwa wa injili tangu Septemba 27 hadi Oktoba Mosi, 2017 katika uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ulioandaliwa na kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola.

Mhe.Mongella aliwahakikishia ushirikiano mwema pindi watakapokuwa tayari kuwekeza katika shughuli mbalimbali ikiwemo za kielimu katika mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani
Wageni kutoka Marekani pamoja na mwenyeji wao Mchungaji Kulola, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani. Katikati ni Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani na kushoto ni Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati), Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani (kushoto) pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia)
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiwa pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia).
Katibu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Levi Matia (kushoto), akiwakaribisha wageni kutoka Marekani walipotembelea ofisini hapo jana.
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani ikiwa kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani ikiondoka katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza na mwenyeji wao Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (wa kwanza kushoto).
Salamu na wenyeji katika mitaa ya Jiji la Mwanza
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani pamoja na wenyeji wao fukwe za Ziwa Victoria ili kujionea mawe ya "Bismarck Rock" katika eneo la Kamanga
Walifurahia uzuri wa eneo hili na hakika hii ni nenmbo ya Jiji la Mwanza
Walifurahia ukaaji wa mawe haya
Pia ilikuwa furaha kugusa maji ya Ziwa Victoria mubashara
Eneo hili lina mijusi wakubwa hivyo walifurahia kuitazama mubashara
Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) kutoka kanisa la kimataifa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, katika fukwe za Kishimba Beach.
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates