Sunday 30 July 2017

MANENO KUNTU KUTOKA KWA MCHUNGAJI KULOLA

Julai 23 hadi jana 30,2017 ulifanyika Mkutano wa Injili ulioandaliwa na Makanisa ya EAGT Kanda ya Kusini Jijini Mwanza, uliofanyika uwanja wa shule ya Msingi Buhongwa.

Mhubiri aliyealikwa kuhudumu kwenye mkutano huo alikuwa Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani juu).

Katika Mahubiri yake, Dkt.Kulola alikuwa akisisitiza zaidi jumbe zenye lengo la kubadili fikra za wanadamu na siyo kuwapotosha kama ambavyo baadhi ya wahubiri wamekuwa wakiwahadaa waumini wao.  
BONYEZA HAPO CHINI KUSIKILIZA MANENO KUNTU YA MCHUNGAJI KULOLA Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Dkt.Daniel Moses Kulola akihubiri kwenye mkutano wa Injili ulioandaliwa na Makanisa ya EAGT Kanda ya Kusini Jijini Mwanza. Mchungaji Mercy Kulola (Mama Mchungaji Daniel Kulola) akiwa kwenye mkutano huo

MAMIA WAFURAHIA NDOA ZA PAMOJA EAGT LUMALA MPYA MWANZA

Jumapili ya wiki mbili zilizopita (Julai 16,2017) zilifungwa ndoa tisa kwa wakati mmoja katika kanisa la EAGT Lumala Mpya, lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza na kuvutia mamia ya watu wakiwemo waumini wa kanisa hilo. 

Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola alisema si vyema waumini waliookoka wakiwa kwenye ndoa bubu kuendelea kuishi ndani ya ndoa hizo bila kufunga ndoa takatifu na hivyo kuwapa fursa ya kipekee wale wote wenye ndoa bubu kufunga ndoa takatifu. 

Shughuli ilikuwa ya kuvutia ambapo baada ya masaa kadhaa video ya mmoja wa waliofunga ndoa siku hiyo ilianza kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikimuonesha akielezea namna alivyofurahi kufunga ndoa. Wanandoa Victor Mwampiki na mkewe Shaniah Nyerii. Wengine na best man na best lady wao. Bwana harusi Amos Severine na mkewe Esther Phabian wakisaini cheti cha ndoa Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses kulola pamoja na Mchungaji Mercy Kulola, wakikata keki kwenye ufunguzi wa hafla ya harusi hizo.

MAMA MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA AHITIMU MASOMO YA UCHUNGAJI

Jana Julai 29,2017 Mchungaji Mercy Kulola akiwa kwenye mahafali yake baada ya kuhitimu masomo ya biblia ngazi ya Diploma, katika chuo cha Biblia St.Paul Jijini Mwanza.

Mama Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Mercy Kulola (pichani juu), jana Julai 29,2017 alitunukiwa Diploma yake ya uchungaji baada ya kuhitimu masomo ya biblima katika Chuo cha Biblia St.Paul Jijini Mwanza ngazi hiyo ya Diploma na sasa ataitwa Mchungaji Mercy Kulola.

Baada ya mahafali yaliyofanyika viunga vya chuo cha St.Paul, waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, walimuandalia hafla ya kumpongeza iliyofanyika kanisani hapo majira ya jioni. BMG tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Mchungaji Mercy Kulola kwa hatua hiyo muhimu katika maisha yake.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola akimpongeza mkewe, Mchungaji Mercy Kulola kwa kuhitimu elimu yake ya uchungaji ngazi ya Diploma, katika Chuo cha Biblia St.Paul Jijini Mwanza
Ndugu, jamaa na marafiki kwenye picha ya pamoja

Monday 10 July 2017

NDOA ZA KIHISTORIA KUFUNGWA SIKU MOJA NDANI YA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Mwenyekiti wa kamati ya harusi (kushoto) na katibu wake.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya waliookoka katika kanisa hilo huku tayari wakiwa wanaishi na wenza wao kama mme na mke bila kufunga ndoa takatifu, wamepata fursa ya kufungishwa rasmi ndoa takatifu.

Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola amesema si vyema waliookoa kuishi kama mme na mke huku wakiwa hawajafunga ndoa takatifu madhabahuni mwa Bwana hivyo jumapili ijayo Julai 16,2017 zitafungwa ndoa za pamoja zaidi ya tisa kwa waumini waliookoka huku tayari wako kwenye ndoa bubu.

"Usikae na mme au mke bila kufunga ndoa, maana ndoa bubu itakukotea puani. Acha kuvaa mapete ya ajabu ajabu bila kufunga ndoa. Unakuta lipete lina kichwa cha nyoka, jiulize hilo lipete umepewa na nani? Huenda ndiyo maana unaandamwa na mapepo". Alisisitiza Dkt.Mchungaji Kulola.

Baadhi ya wanaotarajiwa kufunga ndoa siku hiyo, wamefurahishwa na fursa waliyoipata huku wakisema aina hiyo ya ndoa ni nzuri kwa kuwa hawatatumia gharama kubwa kwani baada ya kufunga ndoa, watapata chakula cha pamoja kanisani hapo na baadaye kurejea nyumbani.

Tukio hilo la kihistoria litaanza saa nane kamili mchana katika kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza na watu wote wanakaribishwa kulishuhudia ambapo baada ya ndoa hizo kufungwa, itafanyika tafrija fupi kanisani hapo ambapo watu watakula na kunywa pamoja na wanandoa hao.

Sunday 2 July 2017

WATUMISHI WA MUNGU KUTOKA MAREKANI WAHUDUMU EAGT LUMALA MPYA.

Mchungaji Ken Maxwell kutoka Florida Marekani akiwa na familia yake hii leo kwenye ibada za kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza. Mchungaji Maxwell na familia yake pamoja na watumishi wengine wa Mungu kutoka Marekani wanaendelea kuhudumu katika kanisa hilo tangu June 27 na watafikia tamati siku ya kesho Julai 03, 2017.

Kuna ibada tatu kila jumapili, ibada ya kiingereza kuanzia saa 12 kamili hadi saa moja kamili asubuhi, ibada ya pili ya kiswahili kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa nne na nusu asubuhi na ibada ya tatu ya kiswahili kuanzia saa nne na nusu asubuhi hadi saa nane kamili mchana.

Usikose kesho kuanzia saa tisa na nusu alasiri, ambapo kutakuwa na mafundisho pamoja na maombezi katika kanisa la EAGT Lumala Mpya ambapo watumishi wa Mungu kutoka Marekani pamoja na watumishi wa Mungu wenyeji kutoka kanisa hilo watakuwepo kukuhudumia kwa jina la Yesu na hakika Bwana atakubariki.
Mchungaji Ken Maxwell (kulia) na mkewe wakitoa salamu zao hii leo 
Mtumishi wa Mungu Glen Elleben kutoka Marekani
Watumishi wa Mungu Glen Elleben (kushoto) na mkewe kutoka Marekani wakisalimia kanisa hii leo
Kutoka kulia ni Mchungaji Daniel Kulola wa EAGT Lumala Mpya na Watumishi waengine  Mungu kutoka Marekani
Kutoka kulia ni Mchungaji Daniel Kulola wa EAGT Lumala Mpya International Church na mkewe pamoja na watumishi wengine wa Mungu kutoka Marekani
Mchungaji Ken Maxwell kutoka Marekani akihudumu kwenye ibada za leo kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza. Kuna ibada tatu kila jumapili, ibada ya kiingereza kuanzia saa 12 kamili hadi saa moja kamili asubuhi, ibada ya pili ya kiswahili kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa nne na nusu asubuhi na ibada ya tatu ya kiswahili kuanzia saa nne na nusu asubuhi hadi saa nane kamili mchana.
Moses Daniel Kulola (kulia) akiongoza ibada ya kwanza ya kiingereza ambayo huanza saa 12:00 asubuhi hadi saa 01:00 asubuhi kila jumapili
Mwimbaji wa nyimbo za injili Sam D (kulia) pamoja na George Binagi kutoks EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza
Wageni kutoka Marekani pamoja na waumini wa kanisa la EAGT Lumala Mpya wakifuatilia ibada za leo jumapili. Kuna ibada tatu kila jumapili, ibada ya kiingereza kuanzia saa 12 kamili hadi saa moja kamili asubuhi, ibada ya pili ya kiswahili kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa nne na nusu asubuhi na ibada ya tatu ya kiswahili kuanzia saa nne na nusu asubuhi hadi saa nane kamili mchana.
Bonyeza HAPA kwa picha zaidi
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates