Waimbaji kutoka Marekani jana jumapili Juni 25,2017 wamerindima kwenye tamasha zuri la Kusifu na Kuabudu katika kanisa la kimataifa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza.
Mbali na waimbaji hao wanaounda kundi la Mercy Band, pia walikuwepo waimbaji kutoka EAGT Lumala Mpya waliojaaliwa karama ya kusifu na kumwabudu Mungu kwa Roho na Kweli na hivyo kufanya tamasha hilo kuwa la kipekee.
Waumini wa kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiongozwa na mchungaji wao, Dkt.Daniel Moses Kulola walifurahishwa na tamasha hilo huku kila mmoja akivutiwa namna waliookoka wanavyomtumikia Mungu kwa ari na nguvu.
Baada ya tamasha hilo, unaanza tena mkuano wa OYES (Open Your Eyes and See-Fungua Macho Yako na Uone) ikiwa ni mkutano wa pili mwaka huu ambapo mkutano huo utaanza kesho Juni 27 hadi jumatatu Julai 03 katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya.
Mchungaji Kulola alisema katika mkutano huo, atakuwepo mhubiri Ken Maxwell pamoja na Mercy Band kutoka Florida Marekani bila kuwasahau waimbaji wa nyumbani kama vile Havillah Gospel Singers, Revival Kwaya, Sam D, David Cosmas, Allen Ndageji, Agness Akrama na Happy Shamawere.
Usikose katika mkutano huo wa OYES ambapo kutakuwa na maombezi pamoja na mafundisho ya neno la Mungu.