Injili inatarajiwa kurindima katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza, kuanzia jumapili ijayo juni 25,2017 kwa kuanza na tamasha la muziki wa injili likiwahusisha waimbaji wa nyumbani na Marekani.
Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake na kwamba watumishi wa Mungu ambao ni pamoja na Glen Elleben, Garry & Christina, Charity Brading, Dylan Smith & Makayla Rodgers wamethibitisha kuwepo kwenye tamasha hilo, siku ya jumapili.
Dkt.Mchunhaji Kulola ameongeza kwamba baada ya tamasha hilo, utaanza mkuano wa OYES (Open Your Eyes and See-Fungua Macho Yako na Uone) ikiwa ni mkutano wa pili mwaka huu ambapo mkutano huo utaanza Juni 27 hadi Julai 03 mwaka huu katika viunga hivyo vya kanisa la EAGT Lumala Mpya.
Amesema mhubiri Ken Maxwell pamoja na Mercy Band kutoka Florida Marekani watahudumu kwenye mkutano huo wa OYES bila kuwasahau waimbaji wa nyumbani kama vile Havillah Gospel Singers, Revival Kwaya, Sam D, David Cosmas, Allen Ndageji, Agness Akrama na Hapy Shamawere.
Usikose kufika katika tamasha hilo la jumapili pamoja na mkutano wa OYES ambapo kutakuwa na maombezi na mafundisho ya neno la Mungu.