Sunday 25 December 2016

IBADA MAALUMU YA KRISMASI, KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LABARIKI WATOTO.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, hii leo Disemba 25, 2016 akihubiri kwenye ibada maalumu ya Krismasi ambayo imeenda sambamba na kubariki watoto ikiwa ni ishara njema katika siku hii ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Somo limetoka Kitabu cha Marko Mtakatifu 10:07.

Ibada hiyo...
Ibada hiyo pia imekuwa njema kwani Mhubiri wa Kimataifa, Josephine Miller kutoka Marekani amehitimisha mahubiri na mafundisho yake ya mwisho ya zaidi ya wiki moja (Disemba 19-Disemba 25) katika Kanisa hilo la EAGT Lumala Mpya.

Mchungaji Miller amefurahishwa na huduma katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya ambapo ametoa rai kwa waumini wote kumtumikia Mungu. Ameonya juu  ya wale wote wasiomwabudu Yesu Kristo aliye kufa na kufufuka na badala yake wanaabudu miungu wengine kwa mwamvuli wa dini kwa mnajiri ya kujipatia pesa. Somo limetoka Kitabu cha Matendo ya Mitume 01:11
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakifuatilia mahubiri kutoka kwa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola.
Miongoni mwa watoto waliobarikiwa hii leo katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, wakiwa wamebebwa na wazazi/walezi wao
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kulia) pamoja na Mama Mchungaji, Mercy Kulola, wakiendelea na ibada ya kuwabariki watoto katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya hii leo.
Baadhi ya akina mama wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani baada ya kumaliza mahubiri na mafndisho yake hii leo.
Akina mama wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani baada ya kumaliza mahubiri na mafndisho yake
Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani akimtakia baraka njema George Binagi, mmoja wa waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya.
Baadhi ya vijana wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani baada ya kumaliza mahubiri na mafndisho yake hii leo.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka EAGT Lumala Mpya, Happy Shamawele, akitumbuiza kwenye ibada ya Krismasi katika kanisa hilo hii leo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kushoto) pamoja na waumini wengine wakifuatilia ibada maalumu ya Krismasi hii leo
Mchungaji Josephine Miller (kushoto) kutoka Marekani pamoja na Mama Mchungaji Mercy Kulola (kulia) wakifuatilia ibada ya Krismasi hii leo
Happness Materego kutoka EAGT Lumala Mpya akifuatilia ibada
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifuatilia ibada
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifuatilia ibada ya Krismasi
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifuatilia ibada ya Krismasi hii leo.
Tunawatakia Krismasi Njema, Sherehekea kwa Amani na Utulivu kwa kuzaliwa Emmanuel (Yesu), Mungu pamoja nasi aliyeuokoa ulimwengu huu. Picha na Craty Cleophace wa EAGT Lumala Mpya kwa ushirikiano na BMG.
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates