Sunday, 20 November 2016

PICHA YA MAREHEMU ASKOFU DR.MOSES KULOLA NA ALIYEKUA SPIKA MSTAAFU MAREHEMU SAMUEL SITTA WALIPOKUTANA

Katika kuonesha kuwakumbuka watu hawa muhimu katika Tanzania, mtoto wa aliyekua Askofu Mku wa kanisa la EAGT nchini Tanzania Dr.Moses Kulola, afahamikaye kama Mchungaji Dr. Daniel Kulola amepost katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook picha akiwa na baba yake "Kulola " na aliyekua Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta siku walipokutana pamoja uwanja wa ndege katika safari .
Itakumbukwa kuwa Askofu Moses Kulola alifariki dunia mwaka 2013 akiacha alama kama Baba wa Injili nchini Tanzania na kiongozi aliyewalea kihuduma watumishi wengi wakubwa na maarufu , huku aliyekua Spika mstaafu Samuel Sitta amefariki mwezi November mwaka huu 2016 na kuacha simanzi nzito kwa taifa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa taifa la Tanzania katika utumishi wake katika serikali.

Thursday, 17 November 2016

MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA ASHEREHEKEA MIAKA 27 YA NDOA YAKE

 Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya jijini Mwanza leo ametimiza miaka 27 ya ndoa na mke wake Bi.Mercy Kulola baada ya kuwa pamoja tangu walipofunga ndoa mwaka 1989.

Katika ukurasa wake wa facebook Dr.Kulola amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa neema na rehema zake alizowajalia katika ndoa yao, huku akielekeza salamu zake za upendo kwa mkewe na msaidizi katika huduma ya uinjilist ambayo wamekua wakiifanya kwa kuzunguka nchi mbalimbali kuhubiri injili katika mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani.

Katika ukurasa wake hiki ndicho alichokiandika Mchungaji Dr.Kulola jr.


ATTENTION PLEASE
Today 18th Nov, is our marriage anniversary, We thank God for His aboundant Grace mercy, and honor in our marriage. You can imaging since 1989 until today 18th Nov 2016 it is by the Grace of God. Let me tell my lovely wife Mercy Daniel that you are everything to me, ilove you, and respect you. Share with us please to say anything


 
 
 


 

MAHUBIRI YA MCH.DR.DANIEL MOSES KULOLA HUKO QUEBEC CANADA


Sunday, 13 November 2016

KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA LAFANYIKA BARAKA KWA WAUMINI WAKE.

 Waumini wa Kanisa la EAGT LUMALA MPYA Jijini Mwanza, wakipata mahubiri, maombi na mafundisho ya mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, katika ibada za jana jumapili, Novemba 13,2016.

Mtumishi huyu amefanyika...

Tuesday, 8 November 2016

MUUMINI WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA ASHUHUDIA UKUU WA MUNGU BAADA YA KUIBUKA MILIONEA NA M-POWER.

Mshindi wa shilingi Milioni 100 kutoka Jijini Mwanza katika promosheni ya M-Power inayosimamiwa na kampuni ya simu ya Vodacom, Mama Paulina Kulwa (kushoto), akiwa na mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola wakati wa kukabidhiwa hundi yake.

Mama Paulina Kulwa (58) ni...

Sunday, 6 November 2016

MAFUNDISHO YA MCHUNGAJI DANIEL KULOLA KUONESHWA KWENYE KING'AMUZI CHA CONTINENTAL.

Usikose kufuatilia mahubiri na mafundisho ya Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia), kwenye runinga ya STAR RELIGION kupitia king'amuzi cha CONTINENTAL.

Ni kila siku za...
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates