Tuesday 20 June 2017

HABARI NJEMA KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

 Injili inatarajiwa kurindima katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu  la Sabasaba Jijini Mwanza, kuanzia jumapili ijayo juni 25,2017 kwa kuanza na tamasha la muziki wa injili likiwahusisha waimbaji wa nyumbani na Marekani.

Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake na kwamba watumishi wa Mungu ambao ni pamoja na Glen Elleben, Garry & Christina, Charity Brading, Dylan Smith & Makayla Rodgers wamethibitisha kuwepo kwenye tamasha hilo, siku ya jumapili.

Dkt.Mchunhaji Kulola ameongeza kwamba baada ya tamasha hilo, utaanza mkuano wa OYES (Open Your Eyes and See-Fungua Macho Yako na Uone) ikiwa ni mkutano wa pili mwaka huu ambapo mkutano huo utaanza Juni 27 hadi Julai 03 mwaka huu katika viunga hivyo vya kanisa la EAGT Lumala Mpya.

Amesema mhubiri Ken Maxwell pamoja na Mercy Band kutoka Florida Marekani watahudumu kwenye mkutano huo wa OYES bila kuwasahau waimbaji wa nyumbani kama vile Havillah Gospel Singers, Revival Kwaya, Sam D, David Cosmas, Allen Ndageji, Agness Akrama na Hapy Shamawere.

Usikose kufika katika tamasha hilo la jumapili pamoja na mkutano wa OYES ambapo kutakuwa na maombezi na mafundisho ya neno la Mungu.
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates