Saturday 30 November 2013

KANALI MSTAAFU MBILIZI KATUTOKA



kanali Shadrack Mbilizi moja wa makanali shupavu wa jeshi la wananchi wa Tanzania amefariki Dunia.
Kwa taarifa ambazo tumezipata kutoka katika vyanzo vyetu vya habari kanali Mbilizi ambaye baada ya kustaafu jeshini mwaka 1988 alirudi kuishi mji mdogo wa Lugeye nje kidogo ya Nyanguge  mkoani mwanza alifariki alfajiri ya tarehe 28 Novemba 2013 katika Hosp ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa.


Habari zimeendelea kuripotiwa alikuwa amepatwa na presha ya ghafla akapelekwa kwa matibabu mjini Magu ambako ilionekana anahitaji matibabu zaidi ndipo alihamishiwa Bugando Hosp... baada ya matibabu alitolewa na kukaa katika moja ya familia ya wanawe ili awe karibu na huduma za hosp siku ya kurudi hosp kwa uchunguzi zaidi. Lakini hali yake ilibadilika ghafla na kurudishwa Bugando hosp na kisha kuwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ambako ndiko mauti ilimkuta tarehe 28 Nov alfajiri.
  Taarifa kutoka kwenye familia inasema aliagizwa kuzikwa kijeshi pindi ikitokea siku moja hayuko duniani.. baada ya kutoka duniani familia iliweka taratibu pamoja na viongozi wa kijeshi.... Marehemu Kanali Mbilizi hadi anatutoka alikuwa na miaka 90 kwani taarifa inaonyesha alizaliwa 27 machi 1923 na kufariki 28 Nov 2013.
Msiba huu mkubwa unagusa familia kubwa za jijini mwanza ikiwa ni pamoja na familia ya marehemu askofu mkuu Dr. Moses kulola. Marehemu kanali Mbilizi ndiye sanji wa Mzee kulola kwa mwanawe Pastor Dr. Daniel Kulola ambaye ameoa kwake.
Kwenye mambo kama haya huwa hapakosekani na mambo ya kushangaza na kufurahisha pia..Tukio la kuashiria mema lilitamkwa na mwongoza mazishi mch na mwinjilisti wa AIC kiongozi wa kanisa marehemu alikuwa akiabudu alipotaka ibada ya mazishi ifunguliwe ,,, kupitia kwenye microphone alitamka tunamkaribisha askofu Dr. Daniel Kulola aje kutufungulia ibada yetu... watu wote wakasema na iwe hivyo... badaa ya mazishi kila mmoja alimfuta mch huyo na kuanza kumpa hongera na kumwambia ndivyo tunataka... ila Mch Daniel Kulola alionekana kunyamaza kimya tu...kidogo akimwangalia mama yake na yeye kusema mapenzi ya Mungu yanaonekana.
Akizungumza kwa huzuni dr Kulola alisema familia imepoteza kiongozi mzuri na shupavu katika nchi na kifamilia pia. Tutazidi kumkumbuka na kuyaenzi mazuri ya kanali alimalizia kwa kusema hivyo.
Marehemu ameacha watoto hai 13 na wajukuu pia watukuu na mke mmoja.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA MBINGUNI---AMEN






 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates