Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, kwenye ibada za leo jumapili, Januari 15,2017.
Kulikuwa na somo zuri liitwalo "KWELI MUNGU YUPO" kutoka kitabu cha 1-Wafalme 18 hivyo soma kwa kitabu hicho ili ujifunze zaidi kuhusiana na uwepo wa Mungu ukimtafuta kwa uaminifu.
Watoto wakimsikiliza kwa makini Mchungaji, Dkt.Daniel Moses Kulola, baada ya kuwaombea ili kuelekea kwenye mafundisho yao
Jumapili ibada ya kwanza huanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 01:00 asubuhi na ibada ya tatu saa 04:30 asubuhi huku ibada za katikati ya juma zikifanyika jumatano na ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, akiwemo mama Mchungaji Mercy Daniel Kulola (katikati), wakiwa kwenye maombi kanisani hapo
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, wakifuatilia ibada kanisani hapo
Hakikisha hukosi ibada za Kanisa la EAGT Lumala Mpya.