Kanisa la kimataifa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, linawakawaribisha watu wote kwenye mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Ilemela.
Mchungaji Kiongozi Dkt.Daniel Moses Kulola pamoja na Mwinjilisti Roggers Mathias kutoka Marekani watahudumu kwenye mkutano huo huku waimbaji mbalimbali kama vile Havillah Gospel Singers, Ambwene Mwasongwe na Sam D wakitumbuiza pia.