Mwenyekiti wa faraja kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kushoto),akimkabidhi muumini wa kanisa hilo George Binagi mchango wa faraja baada ya kufiwa na mama mzazi mapema mwaka huu (Januari 29,2017) kwa niaba ya waumini wengine.
Juzi jumatatu Mei 15,2017 waumini wa kanisa hilo wakiongozwa na Mchungaji wao, Dkt.Daniel Moses Kulola, walifika nyumbani kwa Binagi, Ghana Jijini Mwanza kumfariji na kufanya ibada ya pamoja baada ya msiba ikiwa ni utaratibu wa kanisa hilo kuungana pamoja kwenye shida na raha.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya,Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia), akiwa na Mr. & Mrs. George Binagi
Muumini wa EAGT Lumala Mpya
Familia ya Mr. & Mrs.George Binagi, inatoa shukurani za dhani kwa waumini wote wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Kiongozi, Dkt.Daniel Moses Kulola, kwa upendo wao, Mungu awabariki.