Kila jumatatu saa kumi na mbili kamili jioni hadi saa mbili kamili usiku, huwa kuna majadiliano mubashara kupitia ukurasa wa facebook wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, ambapo mada mbalimbali hujadiliwa.
Leo jumatatu March 13,2017 kumekuwa na mwendelezo wa mada moto isemayo "Wokovu bila umaskini inawezekana". Majadiliano hayo yenye mafundisho mema ya neno la Mungu, pia hurekodiwa kwa ajili ya kurushwa kwenye luninga ya Star Religion kupitia kisimbuzi cha Continental.
Tamati ya mjadala wa leo umedhihirisha kwamba ni kweli kwamba wokovu bila umaskini inawezekana ikiwa tu walio ndani ya wokovu watauelewa vyema wokovu wenyewe. Ufahamu ulio ndani ya wokovu ikiwa utatumika vyema katika kufanya kazi kwa bidii na kumtumaini Mungu, Baraka nyingi zitamiminika kwa waliokoka na Mwenyezi Mungu atawajaza maradufu.
Fanya kazi kwa bidii huku ukimwamini Mungu ndani ya wokovu naye atakubariki maana maandiko matakatifu yanasema atabariki kazi za mikono yako.
Bonyeza hapa kutazama mjadala wa leo na usikose kufuatilia mijada hii inayoongozwa na Mchungaji Daniel Moses Kulola kila jumatatu kupitia BMG.