Tuesday, 27 December 2016

MCHUNGAJI JOSEPHNE MILLER KUTOKA MAREKANI AFURAHIA KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA SERENGETI.

Disemba 19 hadi 25 mwaka huu, Mchungaji Josephine Miller (wa tatu kushoto) kutoka Marekani alikuwa akifundisha na kuhubiri katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza. 

Baada ya huduma hiyo, jana Disemba 27, wenyeji wake (pichani) wakiongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (wa sita kulia) na Mama Mchungaji Mercy Kulola (wa tano kulia), walimtembeza Mchungaji Miller katika hifadhi ya Taifa Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika fidhahi hiyo.
Imeandaliwa na George Binagi, Picha na Jorum Samwel
Wanaumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, baada ya kuwasili katika hifhadhi ya Serengeti
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifurahia uwepo wao ndani ya hifadhi

Sunday, 25 December 2016

MWIMBAJI MAARUFU WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AFUNGA PINGU ZA MAISHA.

Mbali ya kuwa Sikukuu ya Krismasi kwa Wakristo duniani, pia jana Disemba 25,2016 ilikuwa siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine (wawili katikati), baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.

MCHUNGAJI JOSEPHINE MILLER KUTOKA MAREKANI AZUNGUMZIA SIKUKUU YA CHRISMASI.

Mchungaji Josephine Miller (kushoto) kutoka nchini Marekani, akizungumza na George Binagi (kulia), baada ya kuhitimisha mafundisho na mahubiri ya juma zima katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya hii leo.

Amesema Krismasi ni msimu muhimu si tu kwa Amerika bali pia kote ulimwenguni hususani kwa wote wanaomwamini Yesu Kristo aliyezaliwa Bethlehem. Anasema kuzaliwa kwa Yesu Kristo ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa ajili yetu.

Amewatia moyo watanzania kumwamini Mungu kwani yuko pamoja nao, bila kujalisha hali yoyote ile waliyonayo ikiwemo kiuchumi.
Bonyeza HAPA Au play kusikiliza

IBADA MAALUMU YA KRISMASI, KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LABARIKI WATOTO.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, hii leo Disemba 25, 2016 akihubiri kwenye ibada maalumu ya Krismasi ambayo imeenda sambamba na kubariki watoto ikiwa ni ishara njema katika siku hii ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Somo limetoka Kitabu cha Marko Mtakatifu 10:07.

Ibada hiyo...
 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates