UTAFANYIKA NDANI YA KANISA LA MIKOCHENI B' ASSEMBLIES OF GOD 16/3 hadi 23/3/2014
Mhubiri wa kaimataifa na mch wa kanisa la EAGT Lumala Mpya Mwanza Pastor Dr. Daniel Moses Kulola atakuwa na huduma kubwa ndani ya kanisa la Mikocheni B' assemblies Mlima wa Moto chini ya Mch Mhe. Dr. Getrude Rwakatare Dar es Salaam kuanzia tarehe 16/3 hadi 23/3/2014.
Kwa namna tunavyoijua huduma ya mch Dr. Kulola imekuwa ni ya baraka sana mahali kote tunaamini umati mkubwa sana wa watu watafurika katika kanisa hilo.
Tukiongea na mch Kulola, ELM news ilitaka kupata uhakika wa safari hiyo pia na kama kweli huduma hiyo itakuwepo kama vile taarifa zilivyo zagaa mahali kote, Mch Kulola alithibitisha ni kweli na mipango ya maandalizi ya mkutano huo wa ndani zimekwisha anza kufanyika ikiwa ni pamoja na maandalizi ya matangazo na maombi pia.
akizungumza kwa kusisitiza mhubiri huyu wa kimataifa aliwaomba watu wote kufika katika wiki hiyo ya baraka.
Mch Kulola ambaye tangu mwaka jana 2013 Desemba hadi februari 2014 alikuwa marekani kwa huduma ya injili kwenye majimbo kadhaa amekuwa ni mhubiri wa baraka si nchini tu Tanzania lakini pia kwa nchi nyingi za africa mashariki na kati pia nje za ulaya. Ni mtoto pekee wa askofu marehemu Dr. Moses Kulola ambaye ni mchungaji amekuwa ni changamoto kubwa ya injili katika taifa letu la tanzania. Na ndiye mrithi wa huduma ya mzee.