Ndoa ya Mr.Victor Misana pamoja na Miss Queen Mrema imefana leo Jumapili Novemba 12,2017 katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Wawili hao wote ni waumini wa kanisa hilo chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola. Baada ya ndoa hiyo, hafla inafanyika ukumbi wa New Mwanza Hote Jijini Mwanza usiku.
Bwana harusi Victor Misana, akimlaki bibi harusi Queen Mrema. Bwana harusi akithibitisha kuwa ndiye. Maharusi wakiingia kanisani, EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza. Maharusi wakiwa kanisani. Bwana harusi akimvisha pete mkewe.Bibi harusi akimvisha pete mmewe. Maharusi wakionyesha pete za harusi. Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiwaombea maharusi. Mama Mchungaji Mercy Kulola pia akiwaombea maharusi. Kulia ni mwakilishi wa familia ya bibi harusi akimkabidhi kwa wakwe. Kulia ni mwakilishi wa familia ya bwana harusi akizungumza baada ya kumpokea bibi harusi.
Mr. & Mrs Victor Misana Maharusi pamoja na marafiki zao. Maharusi pamoja na wasimamizi wao. Mama Mchungaji Mercy Kulola (kulia) pamoja na wazazi wa bibi harusi.