Thursday, 13 February 2014

UZINDUZI WA KITABU CHA MAISHA NA HUDUMA YA ASKOFU MKUU DR. MOSES KULOLA

UZINDUZI WA KITABU CHA MAISHA NA HUDUMA YA ASKOFU DR. MOSES KULOLA

Kutakuwa na uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa kwa utaalam wa hali ya juu kwa mkataba katika ya mch Dr. Daniel Kulola na kampuni ya Matokeo Publishers ya Dar es Salaam.
Maandalizi ya utayarishwaji wa kitabu hiki umeanza miaka miwili iliyopita kwa usaidizi wa karibu wa marehemu Askofu Moses Kulola.

Taarifa ambazo zimethibitika uzinduzi huo ambao utajumuisha maaskofu, viongozi wa serikali na wana injili wote Tanzania nzima utafanyika Dar es Salaam tarehe  9/3/2014. chini ya Matokeo Publishers. Jiandae kujipatia kitabu hiki. Maelekezo ya maeneo yapi uzinduzi huu utafanya utafahamishwa mapema katika Blog hii ya ELM

MKUTANO MKUBWA WA INJILI NDANI YA MIKOCHENI B' ASSEMBLIES OF GOD

UTAFANYIKA NDANI YA KANISA LA MIKOCHENI B' ASSEMBLIES OF GOD  16/3 hadi 23/3/2014
 Mhubiri wa kaimataifa na mch wa kanisa la EAGT Lumala Mpya Mwanza Pastor Dr. Daniel Moses Kulola atakuwa na huduma kubwa ndani ya kanisa la Mikocheni B' assemblies  Mlima wa Moto chini ya Mch Mhe. Dr. Getrude Rwakatare Dar es Salaam kuanzia tarehe 16/3 hadi 23/3/2014.
Kwa namna tunavyoijua huduma ya mch Dr. Kulola imekuwa ni ya baraka sana mahali kote tunaamini umati mkubwa sana wa watu watafurika katika kanisa hilo.
Tukiongea na mch Kulola, ELM news ilitaka kupata uhakika wa safari hiyo pia na kama kweli huduma hiyo itakuwepo kama vile taarifa zilivyo zagaa mahali kote, Mch Kulola alithibitisha ni kweli na mipango ya maandalizi ya mkutano huo wa ndani zimekwisha anza kufanyika ikiwa ni pamoja na maandalizi ya matangazo na maombi pia.
  akizungumza kwa kusisitiza mhubiri huyu wa kimataifa aliwaomba watu wote kufika katika wiki hiyo ya baraka.
  Mch Kulola ambaye tangu mwaka jana 2013 Desemba hadi februari 2014 alikuwa marekani kwa huduma ya injili kwenye majimbo kadhaa amekuwa ni mhubiri wa baraka si nchini tu Tanzania lakini pia kwa nchi nyingi za africa mashariki na kati pia nje za ulaya. Ni mtoto pekee wa askofu marehemu Dr. Moses Kulola ambaye ni mchungaji amekuwa ni changamoto kubwa ya injili katika taifa letu la tanzania. Na ndiye mrithi wa huduma ya mzee.



 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates