Kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya mch na mhubiri wa kimataifa Dr. Daniel Kulola limeanza semina ya uamsho mkuu ndani ya ukumbi wa kanisa hilo. Mhubiri katika Semina hiyo ni MwinjilistJustine Mpogole kutoka Morogoro.
Semina hiyo ikipambwa na vinjonjo vya waimbaji kemkem kama vile Agnes Akrama mama wa kuwekeza kwa Yesu, bila kumsahau Happy Shamawele ambaye wiki iliyopita alikuwa kwenye Huduma jijini Kigali nchini Rwanda. Wengine ni Sarah Emanuel huyu naye ni hatari anaimba kwa utulivu mkuu lakini watu wakibarikiwa sana, Agnes Mpangala ambaye naye wiki iliyopita alikuwa Nairobi nchini Kenya. Hao ni waimbaji mmoja mmoja.
Kwa habari ya Makundi kuna kundi matata kabisa kwanya ya Uinjilisti, Ufunuo na Kwaya inayo kuja kwa kasi sana ya Hot spear singers. Mwitikio umekuwa wa kushangaza kwani watu wamekuwa ni wengi sana sana. Ni ombi letu tu kuwa nafasi bado ipo watu wafike kujilisha neno la Mungu.
Kanisa liko nyuma ya soko jipya la Saba saba Lumala, Mwanza.
Kwa mawasiliano, wasiliana na mch mwenyeji Dr. Daniel Kulola - 0767 749040