Sunday, 29 December 2013

On Going Church Rehabilitation in our church E.A.G.T Lumala mpya,Mwanza ,Tanzania

The EAGT Lumala Mpya Church is undergoing Church Rehabilitation for the purpose of expanding the Church Building and be able to accommodate as many people as possible who are currently rapid increasing in great number after being preached in our Gospel outreach campaign that is going on monthly.

The following are the photos that were taken demonstrating the expansion of the Church building from the ordinary one that is being used for weekly Church Services.






























Friday, 27 December 2013

Safari ya Mchungaji Dr.Daniel Moses Kulola America

Mchungaji Dokta Daniel Moses Kulola hivi sasa yupo nchini Marekani ambapo yupo kwa ajili ya huduma katika kumtangaza Yesu Kristo na kuwafikia watu wengi duniani,akiwa huko anatarajiwa kuhudumu katika makanisa mbalimbali katika majimbo tofauti tofauti.

hizi ni baadhi ya picha za Mchungaji Daniel Kulola akiwa nchini Marekani.


Saturday, 14 December 2013

Mch na mhubiri wa kimataifa Dr.Daniel Moses Kulola aondoka mwanza leo kuelekea marekani

 

Mch na mhubiri wa kimataifa Dr.Daniel Moses Kulola aondoka mwanza leo kuelekea marekani, kafikia hotel ya kimataifa ya JB BELMONTE ya jijini Dar es salaam akijitayarisha na safari yake ya kesho mchana saa saba kuelekea Doha alafu Washington DC kuubiri injili..Yeye akiwa kama kijana pekee aliyeachiwa kijiti na baba yake mzazi,the late Bishop Moses Kulola kuisambaza habari iliyo ya kweli kwa watu wote na wapate kupona

Dr.Mchungaji Daniel Kulola kuanza kuhubiri kwa njia ya Radio kupitia Radio Free Africa

Daktari na Mchungaji Daniel Moses Kulola akiwa katika kituo cha kurusha matangazo cha RFA (radio free Afrika) katika kipindi kipya cha dini ambacho kitaanza kurushwa jumapili hii kuanzia saa kumi na moja alfajiri hadi saa kumi na mbili asubuhi. Na mch. Daniel M. Kulola atahubiri katika kipindi hiki. TUNE 88.8 FM kwa wakazi wa Mwanza na mikoa yote mnayo ikamata radio free africa fungua na utabarikiwa na neon la Mungu pia na uimbaji 

Saturday, 30 November 2013

SEMINA MOTO MOTO - EAGT LUMALA MPYA, JIJINI MWANZA

Kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya mch na mhubiri wa kimataifa Dr. Daniel Kulola limeanza semina ya uamsho mkuu ndani ya ukumbi wa kanisa hilo. Mhubiri katika Semina hiyo ni MwinjilistJustine Mpogole kutoka Morogoro.

Semina hiyo ikipambwa na vinjonjo vya waimbaji kemkem kama vile Agnes Akrama mama wa kuwekeza kwa Yesu, bila kumsahau Happy Shamawele ambaye wiki iliyopita alikuwa kwenye Huduma jijini Kigali nchini Rwanda. Wengine ni Sarah Emanuel huyu naye ni hatari anaimba kwa utulivu mkuu lakini watu wakibarikiwa sana, Agnes Mpangala ambaye naye wiki iliyopita alikuwa Nairobi nchini Kenya. Hao ni waimbaji mmoja mmoja.

Kwa habari ya Makundi kuna kundi matata kabisa kwanya ya Uinjilisti, Ufunuo na Kwaya inayo kuja kwa kasi sana ya Hot spear singers. Mwitikio umekuwa wa kushangaza kwani watu wamekuwa ni wengi sana sana. Ni ombi letu tu kuwa nafasi bado ipo watu wafike kujilisha neno la Mungu.

Kanisa liko nyuma ya soko jipya la Saba saba Lumala, Mwanza.

Kwa mawasiliano, wasiliana na mch mwenyeji Dr. Daniel Kulola - 0767 749040

MHUBIRI WA KIMATAIFA DR. DANIEL MOSES KULOLA KUZURU MAREKANI MWEZI WA DECEMBA 2013

Pastor na mwinjilisti wa Kimataifa ambaye ndiye mtoto pekee ambaye amerithi huduma na majukumu ya askofu mkuu marehemu   Dr Moses Kulola aitwaye Dr. Daniel Moses Kulola amepata mwaliko wa kuelekea Washington Dc Marekani.Ataanzia Boston,kisha Washington DC,Alabama,Dallas,Texas Austin,New york na mahali pengine hakuweza taja kwa huduma ya mwezi mmoja na nusu kuanzia 17 Desemba hadi 30 january 2014.
Akieleza juu ya safari hii kubwa kuwa muda mwingi amekuwa akialikwa kwenda marekani lakini kuna mambo mengi yalikuwa yanaingilia kati kuwa kizuizi. Lakini baada ya mazishi ya baba yake ambaye ni baba yetu sote ameona ni vyema kusafiri kwenda katika huduma maana wengi wamekuwa wakimuhitaji katika nchi hiyo iliyojaa mambo mengi.
Dr. Daniel kulola amekuwa ni moja wa wahubiri wachache ambao wamepata neema ya kipekee ya kwenda kuhubiri katika nchi nyingi zilizoendelea kama uingereza, ujerumani, Dernmark na kwingineko kwingi. Na taarifa ambazo tumeendelea kuzifuatilia kwa karibu ni kuwa kwa sasa ndiye mhubiri pekee ambaye ameweza kutunza na kuzifuata nyayo za askofu mkuu marehemu Moses kulola na pia ndiye mwenye kibali kikubwa hasa katika makanisa ya EAGT.

KANALI MSTAAFU MBILIZI KATUTOKA



kanali Shadrack Mbilizi moja wa makanali shupavu wa jeshi la wananchi wa Tanzania amefariki Dunia.
Kwa taarifa ambazo tumezipata kutoka katika vyanzo vyetu vya habari kanali Mbilizi ambaye baada ya kustaafu jeshini mwaka 1988 alirudi kuishi mji mdogo wa Lugeye nje kidogo ya Nyanguge  mkoani mwanza alifariki alfajiri ya tarehe 28 Novemba 2013 katika Hosp ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa.

 

Sample text

Welcome note

Dear our Brethren in Jesus Welcome to our website. We are so glad that you have chosen to visit our site. On this site you will be able to know us, our values and challenges as a church family, activities and our weekly and even Yearly program and what the Lord is doing through us here in EAGT Lumala mpya church , Mwanza, Tanzania. Our prayer is that as you browse through this website, the Lord will speak to you so that you may partner with us in prayer and any other way that He may lead you to. Let us join hands as we seek to fulfill the mission and vision that God has given us. Let us redeem the time, before the Lord of times returns. Again welcome. Yours in God’s service, Pastor Dr. Daniel Moses kulola.

Sample Text

 
Blogger Templates